Mshambuliaji Mauro Zarate ameihama klabu ya West Ham inayocheza Ligi Kuu ya Uingereza na kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 alijiunga na West Ham kutoka Velez Sarsfield majira ya joto 2014.
Alitatizika kupata nafasi timu ya kwanza na baadaye akapelekwa QPR kwa mkopo.
Zarate, ambaye ni mzaliwa wa Argentina, alirejea msimu huu na kufana sana Upton Park.
Amefungia klabu hiyo mabao 21 msimu huu.
"West Ham ingependa kumshukuru sana Mauro kwa juhudi zake akiwa na jezi za klabu hii na inamtakia kila la kheri,” klabu ya West Ham imesema kupitia taarifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni