RONALDO KWA KIPINDI CHA SIKU TANO HIZI AVUNJA REKODI HIZI TAMU

Kwa muda wa takribani siku tano gwiji wa soka wa Ureno na Real Madrid avunja rekodi mbalimbali katika ligi ya Hispania na ligi ya Ulaya maarufu kama UEFA CHAMPION LEAGUE



1.RONALDO afunga magoli 30 katika ligi ya La Liga kwa misimu sita mfululizo

   Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza katika ligi ya Hispania kuweza kufunga magoli 30  ndani   ya sita mfululizo akiwa na klabu yake ya Real Madrid na alivunja rekodi hiyo baada ya kushinda goli kati ya Real Madrid wakipambana na Eibar katika dimba la Santiago Bernabeu


2.Afikia rekodi ya Lionel Messi ya kufunga Hat Trick 5 katika ligi ya Mabingwa Ulaya

Ronaldo alifunga Hat Trick yake hiyo jana dhidi ya Vfl Wolfsburg na kuwaacha watu mbalimbali midomo wakiwa hawaamini kilichotokea usiku huo wa jana na kupeleka furaha Santiago Bernabeu.Baada ya Ronaldo kuvunja rekodi anatizamia kuweza kuvunja rekodi nyingine zote zilizowekwa lakini ni ngumu kuvunja rekodi ya Pelle


3.Awa mchezaji wa kwanza kufunga Hat Trick 3 katika msimu mmoja katika ligi ya UEFA

Ronaldo ameweza kufunga Hat Trick 3 katika ligi ya mabingwa ulaya msimu huu na kuweka rekodi ambayo hakuna mchezaji aliyewahi kuiweka katika dunia hii ya sasa na zamani.Baada ya Ronaldo kufunga Hat Trick hiyo pia ameweza kuweka rekodi nyingine je ni ipi hiyo fuatilia


4.Awa fowadi anayeongoza kwa magoli kuliko mafowadi wote wa karne ya sasa

Mpaka sasa Ronaldo ametimiza magoli 501 katika maisha yake ya soka mpaka sasa na kumuacha Lionel Messi ambaye ndiye mpinzani wake mkuu akiwa na magoli 467 hivyo kuwa kinara wa mabao kwa mafowadi wote wa duniani kwa sasa

PIA CRISTIANO RONALDO AMEVUNJA REKODI NYINGI MBALIMBALI TAFADHALI UNGANA NAMI ILI KUPATA MWENDELEZO WA MAKALA HAYA YA REKODI ZA RONALDO THE BEST FOWARD



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

1 maoni:

  1. WynnBET Casino: Online Gaming and Slots in Colorado
    The WynnBET online 충청남도 출장마사지 gaming and slots is one of the fastest growing brands in 원주 출장샵 the gaming industry. A trusted global leader in 상주 출장마사지 online 여주 출장샵 gaming, the WynnBET 제주도 출장샵

    JibuFuta