Usiku wa jana ulikuwa wa Cristiano Ronaldo – magoli yake matatu yakaiwezesha Real Madrid kusonga hatua ya nusu fainali kwa mara 6 mfululizo.

Hii ni fedha ambayo Real Madrid wanapata kwa kufanikiwa tu kuingia kwenye hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League.
Ripoti zinaeleza mchanganuo wa fedha hizo ni 5.6m kwa kuingia nusu fainali — na £1.2m kwa kushinda mechi ya jana usiku.

Mabingwa wa mara 10 wa Champions League walifungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza huko Ujerumani, kabla ya hat trick ya Ronaldo jana kuwaingiza katika listi ya vilabu 9 tu vilivyowahi kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata baada ya kukubali kipigo cha 2-0 au zaidi katika mchezo wa kwanza wa Champions League.
Magoli yake ya jana yamemfanya atimize magoli 16 msimu huu – hii ni mara ya pili kwake kufanikiwa kuvuka magoli 15 kwa msimu mmoja wa Champions League – hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivi.

Ronaldo sasa anakuwa mchezaji pekee kufanikiwa kufunga hat tricks 3 katika msimu mmoja.
Kingine kikubwa – Ronaldo mpaka sasa ana magoli 46 msimu huu katika mashindano yote – amebakisha magoli 4 tu afikie rekodi ya Pele ya kufunga magoli 50 au zaidi kwa misimu 6 mfululizo.
0 maoni:
Chapisha Maoni