Mshambuliaji wa Uganda Farouk Miya, anayechezea taifa hilo michuano ya CHAN inayoendelea Rwanda, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Standard Liege ya Ubelgiji.
Kwa sasa amekuwa akichezea klabu ya Vipers Sports Club.
Klabu hizo mbili zimekubaliana uhamisho wake dola za Kimarekani 400,000 na mkataba unatarajiwa kutiwa saini baada ya michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani.
Miya, 19, aliwafungia Uganda penalti na akasaidia ufungaji wa bao la pili mechi yao ya kwanza CHAN ambayo walitoka sare ya 2-2 na Mali.
Hata hivyo, hataweza kucheza Jumamosi dhidi ya Zambia kama tahadhari baada yake kutatizwa na bega.
Msimu uliopita, Miya alifunga mabao 11 na kusaidia ufungaji wa mengine saba huku akisaidia Vipers kushinda taji la ligi kuu ya Uganda.
Amekuwa katika klabu ya Vipers kwa miaka miwili.
0 maoni:
Chapisha Maoni