Mwingereza Andy
Murray amemshinda raia wa Australia Sam Groth na kufika raundi ya tatu
ya mashindano ya tenisi ya Australian Open.
Mchezaji huyo
aliyeorodheshwa nambari mbili katika mashindano hayo, alimshinda Groth
kwa 6-0 6-4 6-1 katika kipindi cha saa moja na dakika 30.Groth, 28, hakupewa nafasi ya kutawala na Murray, ambaye anatokea Scotland.
Murray, 28, sasa ameingia katika 32 bora ambapo atakutana na Mreno Joao Sousa kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne.
Mwingereza mwingine Johanna Konta alimshinda Zheng Saisai kutoka Uchina 6-2 6-3 na kufika raundi ya tatu ya mashindano hayo upande wa wanawake.
0 maoni:
Chapisha Maoni