PATO WA AC MILAN NJIANI KUTUA CHELSEA
-Straika wa Brazil Alexandre Pato ameridhiana na Chelsea ili kuungana nao kutoka Klabu yake ya Brazil, Corinthians.
Pato, mwenye Miaka 25, aliwahi kung’ara mno na kuonekana kama ndie Staa mpya wa Brazil kwa kuichezea Mechi 27 na kufunga Bao 10 lakini nyota ikafifia na hajaitwa tena kuichezea Nchi yake tangu 2013.
Pato alijiunga na AC Milan ya Italy Mwaka 2007 kutoka Internacional ya Brazil na kufunga Bao 16 kwenye Mechi 43 za Serie A lakini baadae akafifia na Januari 2013 akarejea kwao Brazil kujiunga na Corinthians.
Corinthians wakamtoa kwa Mkopo kwa Sao Pulo kwa Msimu wa 2014/15 na akafunga Bao 19 katika Gemu 59.
KLABU ya Chelsea pia inadaiwa kutaka kusajili wachezaji watatu ambao ni Alexandre Pato, Aymen Abdennour na Alex Teixeira kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi huku wakiwaruhusu Papy Djilobodji na Charly Musonda kuondoka kwa mkopo.
0 maoni:
Chapisha Maoni