Majonzi mfululizo yameikuta familia ya staa mkubwa wa muziki duniani na mwenye heshima pamoja na ushindi wa Tuzo nyingi kubwa, kwanza ilikuwa msiba wa mume wake Rene Angelil ambaye aliugua ugonjwa wa kansa… siku chache baadaye akapata msiba mwingine wa kaka yake, Daniel Dion, na yeye tatizo lilikuwa hilohilo la kansa.
Ndugu jamaa na watu wa karibu wamekutana jana January 21 2016 katika kanisa laNotre-Dame Basilica lililopo nyumbani kwao Montreal, Canada kwa ajili ya shughuli za kuaga mwili wa mume wa mwanamuziki huyo.
Hizi hapa baadhi ya picha na video ya tukio hilo.
Video yenyewe hii hapa, Celine Dion na ndugu zake walivyokutana kuaga mwili safari ya mwisho ya Rene Angelil… RIP Rene Angelil
0 maoni:
Chapisha Maoni