
Staa wa Real Madrid na mshindi wa
pili katika tuzo za Ballon d,or 2015, Cristiano Ronaldo (pichani)
ameweka wazi kuwa kocha mpya wa timu hiyo, Zinedine Zidane anaeleweka na
wachezaji wa klabu hiyo kuliko kocha aliyekuwepo awali, Rafa Benitez.
Akizungumza baada ya mchezo wa ligi
kuu ya Hispania dhidi Sporting de Gijon, Ronaldo alisema tangu nafasi ya
kocha kuchukuliwa na Zidane kumekuwepo na mabadiliko katika klabu hiyo
hali inayochangia kupata ushindi mkubwa katika michezo yote miwili
ambayo amewaongoza Zidane.
“Tunamwelewa zaidi Zidane, na hilo
ndiyo soka.… nimeona mabadiliko tangu alipowasili Zidane lakini wote
Zidane na Benitez wanataka vitu vizuri kwenye klabu,
“Ninajihisi vizuri zaidi nikifundishwa na Zizou na usiniulize kwanini,” alisema Ronaldo.
Aidha Ronaldo alimlinganisha Zidane
na Carlo Ancelotti ambaye aliisaidia Real Madrid kushinda kombe la Ligi
ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2013/2014.
“Ninaona kivuli cha Carlo ndani ya
Zidane, ni mtu ambaye yupo makini na kazi yake wakati wa kufanya kazi na
mcheshi mnapokuwa nje ya kazi,” alisema Ronaldo.
0 maoni:
Chapisha Maoni