
Kiiza alipachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Daniel Lyanga kuangushwa kwenye eneo la 18 la JKT Ruvu kisha mganda huyo kuukwamisha mpira kambani ikiwa ni dakika ya nane kipindi cha pili.

Dakika ya 27 kipindi cha pili, Daniel Lyanga aliihakikishia Simba ushindi baada ya kupachika bao la pili na la ushindi akitumia makosa ya mabeki wa JKT Ruvu waliokuwa wakiugombe mpira mrefu uliopigwa kutoka eneo la Simba. Mabeki hao walishindwa kuudhibiti mpira huo hatimaye ukamkuta Lyanga ambye moja kwa moja aliuweka wavuni.
Ushindi wa leo unaifanya Simba kufikisha pointi 33 nyuma ya mahasimu wao Yanga bado wanapointi zao 36 huku wakisubiri kucheza mechi yao ya kesho dhidi ya Majimaji wakati Azam yenye pointi 39 inakaa kileleni mwa ligi baada ya ushindi wa leo dhidi ya Mgambo JKT uliochezwa jijini Tanga.

Endapo Yanga wakishinda mchezo wao wa kesho watafikisha pointi 39 sawa na Azam FC na kuongoza tena ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Lakini kama watatoka sare au watafungwa basi watawaachia Azam usukani wa kuongoza ligi.

Leo January 20, 2016 imepigwa jumla ya michezo mitatu ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Tanzania bara kwenye viwanja vya miji tofauti. Hapa chini kuna matokeo ya michezo mingine iliyohezwa leo.
Mgambo JKT 1-2 Azam FC (Mkwakwani Stadium-Tanga)
Ndanda FC 4-1 Mbeya City (Nangwanda Sijaona-Mtwara)
Standa United 2-1 Toto Africans (Kambarage Stadium-Shinyanga)
Tanzania Prisons 2-1 Coastal Union (Sokoine Stadium-Mbeya)
Kesho itapigwa michezo mingine mitatu kwa
ajili ya kukamilisha duru la kwanza la ligi kuu Tanzania bara ambapo
mechi hizo zitakamilisha mechi 15 za kwanza za ligi msimu huu kisha
kupisha ratiba ya michuano ya FA kisha kuanza kupigwa michezo mingine ya
lala salama ya ligi hiyo.
Ratiba ya mechi zitakazopigwa kesho ni kama ifuatavyo:
Mwadui FC vs Kagera Sugar
African Sports vs Mtibwa Sugar
Yanga SC vs Majimaji FC
0 maoni:
Chapisha Maoni