TANZIA: SWAI AFARIKI DUNIA
-SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linasikitika kutangaza kifo cha Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo Epaphra Swai ambaye amefariki dunia leo katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alisema kuwa wamepokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo kwani pengo kwao TFF na Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu.
“Swai amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam na sisi TFF tunasikitika kumpoteza kiongozi huyu kwani alikuwa chachu ya maendeleo ya soka”, alisema Malinzi.
Swai atasafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao Machame, wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
0 maoni:
Chapisha Maoni