SHIRIKISHO la Soka Tanzania, linasikitishwa na hali ya uendeshwaji wa soka la Zanzibar baada ya kujitangaza kwa kamati ya muda ya uendeshaji ligi.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana,Rais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amesema amesikitika kusikia kwenye radio
watu wanajiita kamati ya muda ya uendeshaji wa ligi Zanzibar ikisema wametoa
vifaa kwa klabu za Mafunzo na KMKM kwa ajili ya kujiandaa kwa mashindano ya
kimataifa.
“Baada ya kusikia
kuna kesi mahakamani tuliaiandikia ZFA barua yenye namba ya kumbukumbu
TFF/ZFA-03/2015, tukieleza jinsi shirikisho linavyosikitishwa na kuwepo kwa
kesi dhidi ya ZFA”.
Malinzi alisema
awali baada ya kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa ZFA kilichofanyika, Dar es
Salaam chini ya Uenyekiti wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi baada ya kuwepo tishio la Shirikisho
la Soka Afrika (CAF) kuifungia Zanzibar kwenye soka ya kimataifa baada ya
kufikishana Mahakamani, jambo ambalo ni kinyume na sheria za FIFA.
Pia katika kikao
hicho Chama cha
Soka Zanzibar (ZFA), kiliagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura
kujadili mwenendo wa Kamati ya Utendaji na mambo mengine kadhaa ikiwa ni
pamoja na kwenda kufuta kesi zote mahakamani jambo ambalo lilitendeka na
kujibiwa kwa maandishi na ZFA.
Pia Malinzi amesema
amemwagiza Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa kumwandikia barua Rais wa ZFA, Ravia
Idarus, akimtaka amjulishe kama yeye ndiye anasimamia na kuendesha mambo ya
soka visiwani humo ili waijulishe CAF waweze kuchukua hatua kwani ZFA ni
mwanachama wa wake.
Klabu za Chuoni na
Aluta ndizo zilizofungua mashtaki mahakamani wakimtuhu Rais wa ZFA, Ravia Idarus,Makamu
wa ZFA toka Pemba, Ally Mohamed pamoja na Katibu Mkuu, Kassim Haji Salum
kukiuka kanuni za mashindano.
0 maoni:
Chapisha Maoni