Bondia wa Uingereza Anthony Joshua anatarajia kupigana na bondia bingwa wa IBF Charles Martin katika uzito wa Heavyweight mjini London Arena tarehe 9 Aprili.
Mmarekani Martin mwenye miaka 29, ambaye mpaka sasa ameshinda mara 23 na kutoka sare mara moja katika mapambano yake 24, akifanikiwa kumpiga bondia Vyacheslav Glazkov mnamo mwezi Januari.
Kwa upande wake Bondia Joshua mwenye miaka 26, hivi karibuni alifanikiwa kumpiga Dillian Whyte katika uzito wa Heavyweight.
0 maoni:
Chapisha Maoni