Straika wa Leicester City, Jamie Vardy, akiifunga timu yake bao kwa njia ya mkwaju wa penalti dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Emirates. Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Straika wa Arsenal, Danny Welbeck (kushoto) akishangilia bao la ushindi aliloifungia timu yake dhidi ya Leicester City. Kulia ni Alexis Sanchez.
Vardy akipongezwa na mchezaji mwenzake, Marc Albrighton baada ya kufunga bao kwa penalti dhidi ya Arsenal.
Mchezaji wa Leicester, Luke Simpson akimzuia Mesut Ozil wa Arsenal.
Simpson (17) akioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi, Martin Atkinson baada ya kumchezea vibaya Olivier Giroud wa Arsenal.
Theo Walcott (14) akiifungia Arsenal bao la kusawazisha dhidi ya Leicester.
Walcott (katikati) akishangilia bao lake pamoja na Sanchez (kushoto) na Ozil.
0 maoni:
Chapisha Maoni