FA CUP:LEO NI YANGA NA MLALE JKT

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, timu ya Yanga SC Leo Jumatano wataikaribisha JKT Mlale ya Ruvuma katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya kombe la FA. Bingwa wa michuano hiyo ya kombe la TFF ataiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baadaye mwaka ujao.
Yanga ambayo inaongoza msimamo wa VPL (kabla ya mechi ya Tanzania Prisons v Azam FC itakayochezwa Jumatano hii) imepania kushusha kikosi chao kamili dhidi ya timu hiyo ya daraja la kwanza.
“Tumejiandaa vizuri kwa mchezo wetu wa Jumatano wa kombe la FA. Kama unavyofahamu bingwa wa michuano hii ataiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa hapo mwakani hivyo lengo letu ni kufanya vizuri na kushinda mchezo huu”, anasema, Jerry Muro mkuu wa kitengo cha habari wa klabu hiyo bingwa mara 24 ya Bara.
“Tunatarajia kushusha kikosi chetu kamili na mwalimu ana wigo mpana wa kufanya machaguo ya wachezaji.” Yanga itacheza ma Joachim ya Mauritius mwishoni mwa wiki hii katika mchezo wa marejeano  wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya awali.
“Tunajiandaa vizuri na mchezo wa klabu bingwa ambao uongozi wamekubaliana uchezwe siku ya Jumamosi.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni