Mbunge adatishwa na penzi la Lungi

IMG_1632Msanii maarufu wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.


 
Taarifa ambayo gazeti hili linayo ni kuhusu mbunge moja machachari sana wa chama tawala (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye kwa muda mrefu amekuwa akidaiwa kutoka kimapenzi kwa siri na msanii maarufu wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.
Chanzo makini ambacho kipo karibu na Lungi kimeeleza kuwa, Lungi na mheshimiwa huyo wamekuwa ‘lovers’ kiasi cha kufikia kila mmoja kufa na kuoza kwa mwenzake.
Kisikie chanzo
“Yaani suala la mheshimiwa (anataja jina la mbunge huyo) kutoka na Lungi siyo siri na wakati mwingine Lungi mwenyewe anajitapa kuwa sasa hivi ni matawi ya juu, nyie fuatilieni mtajua ukweli.”
Ijumaa laingia mzigoni
Kufuatia madai hayo, Ijumaa liliingia mzigoni kujaribu kuwafuatilia wawili hao hasa inapobainika mheshimiwa huyo yuko jijini Dar lakini hawakuweza kunaswa, hali iliyoonesha kuwa, huwa wanakutana kwa siri sana.
Hata hivyo, rafiki huyo wa Lungi juzikati alimpigia simu mmoja wa waandishi wa Ijumaa na kumueleza kuwa, amefanikiwa kunasa mawasiliano ya Lungi na mheshimiwa.
Mtoa habari huyo akasema kuwa, alifanikiwa kupata sms za kimapenzi ambazo Lungi alikuwa akitumiana na mbunge huyo huku wakati mwingine wakitumiana picha za kihasara.
Kwa makubaliano maalum, chanzo hicho kilikubali kutoa ushahidi huo ambapo Ijumaa lilijiridhisha kuwa Lungi na mbunge huyo wanatoka.
Katika meseji hizo ambazo baadhi ni zile zinazopatikana ukurasa wa mbele, zipo ambazo mheshimiwa huyo anamtaka Lungi amtumie picha na Lungi anafanya hivyo huku mara nyingi wawili hao wakitumia lugha chafu inayoonesha kuwa wamezoeana sana.
Ijumaa lamsaka Lungi
Kufuatia kupatikana kwa sms hizo, waandishi wetu walimtafuta Lungi kupitia simu yake ya mkononi ambapo alisema, anachojikua simu yake ilipotea hivyo huenda kuna mtu anataka kumtibulia.
Ijumaa: Inavyoonekana unatoka na mheshimiwa (anatajiwa jina) na kuna sms tumezipata unachati naye, tena za kingono, unalizungumziaje hilo?
Lungi: Jamani mkitoa hiyo habari mtakuwa mmehusika kwenye wizi wa simu yangu, hayo mambo ya mheshimwa na mimi yanawahusu nini, je kama alikuwa akichati na rafiki yangu mna ushahidi gani kama ni mimi?
Ijumaa: Tunataka kujua tu kama ni mtu wako.
Lungi: Achaneni na mimi (akakata simu).
Mheshimiwa yuko bize
Baada ya Lungi kujitetea kwa staili hiyo, Ijumaa lilijaribu kumpigia simu mheshimiwa mbunge lakini mara nyingi haikupolewa kuonesha kuwa yuko bize na vikao vya bunge vinavyoendelea mkoani Dodoma.
Jitihada za kumtafuta zinaendelea na tutakapompata, tutaanika kila kitu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni