
Mvulana wa taifa la
Afghanistan ambaye aligonga vichwa vya mitandao ya kijamii alipovaa
fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la Lionel Messi hatimaye
amepata jezi nzuri kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Argentina.
BBC ilimsaidia Messi kumtafuta mtoto huyo ambaye anajulikana kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Argentina.Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka 5, anatoka katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

''Ninampnda Messi na fulana yangu inasema Messi ananipenda,Murtaza alisema,tayari akimuigiza mshambuliaji huyo anavyosheherekea bao lake.
Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja ilioenea katika mitandao ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.

0 maoni:
Chapisha Maoni