Umri wa kati ya
miaka 65 na 79 ndio ulio na raha tele miongoni mwa watu wazima
,kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la utafiti wa takwimu za
kitaifa nchini Uingereza.
Utafiti huo uliofanyiwa zaidi ya watu
300,000 nchini Uingereza ulibaini kwamba kujikimu kimaisha ,furaha na
kujihisi unaishi vyema vyote vilipatikana katika umri huo ,lakini furaha
hiyo ikaisha kufikia mwaka wa 80.Wale walio na umri kati ya 45 na 59 waliripoti viwango vya chini vya kujikimu kimaisha, huku wanaume wakijihisi hawafurahi ikilinganishwa na wanawake.
Umri huo pia uliripoti visa vingi vya kuwa na wasiwasi.wanasayansi wa Navu wameelezea vile furaha hubadilika kulingana na umri.
Utafiti huo uliwauliza watu kupima kati ya kiwango cha 10, wana raha kwa kiwango gani na wamekuwa na wasiwasi wa kiwango gani katika siku moja iliopita,wanahisi vipi kuhusu kujikimu kimaisha na kwa kiwango gani wanaona kwamba kile walichokitenda kina thamani maishani.
0 maoni:
Chapisha Maoni