Mcheza Tenisi Mwingereza Andy Murray ametupwa nje katika michuano ya wazi ya Miami na Grigor Dimitrov.
Murray ametolewa katika raundi ya tatu kwa 6-7, 6-4, 6-3, sawa na alama (1-7 ).
Murray mwenye miaka 28, alianza kwa kasi ya juu katika mchezo huo na hadi mapumziko alikuwa akiongoza kwa seti moja.
Lakini Mbulgaria Dimitrov mwenye miaka mika 26 alirejea uwanjani na kumdhibiti Murray na kushinda katika mchezo huo.
Katika mchezo wa awali, Johanna Konta alikuwa mwanamke Mwingereza wa kwanza Kutinga hatua ya robo fainali katika Miami, huku Heather Watson akipoteza kwa Simona.
0 maoni:
Chapisha Maoni