WAKATI England ikijitayarisha kuivaa Netherlands Jumanne Uwanjani Wembley Jijini London kwenye Mechi ya Kirafiki ikiwa ni mara tu baada ya kuwachapa Mabingwa wa Dunia Germany 3-2 Juzi huko Berlin, Meneja wa England Roy Hodgson amelazimika kumtetea Kepteni wake Wayne Rooney ambae hayuko kwenye Kikosi hiki kutokana na kuwa majeruhi.
Wakicheza bila ya Rooney, Vijana wa England kina Harry Kane, Jamie Vardy na Eric Dier walitoka nyuma kwa Bao 2-0 na kuipiga Germany Bao 3-2.
Ushindi huo umezua mjadala huko England huku baadhi ya Watu wakitaka Rooney, ambae ndie Mfungaji Bora katika Historia ya England, amwagwe kwenye Timu.
Akihojiwa kama moto wa Vijana hao wa England utamfanya ampige chini Rooney, Hodgson alijibu: "Sifurahishwi ikiwa wakati huu kaumia Watu wanatajwa kumwagwa kwake. Nina furaha Welbeck amepona na amerejea vizuri, Kane yuko safi. Nina hakika Wayne akipona tutamtathmini."
Aliongeza: "Yeye ni Kepteni wetu. Ameiongoza Timu vyema kwa Miaka Miwili sasa na tumeshinda Mechi 10 kati ya 10 katika Kundi letu la EURO 2016. Hastahili kuhojiwa nafasi yake katika Timu!"
KIMATAIFA KIRAFIKI
Jumanne Machi 29
1900 Estonia v Serbia
1900 Montenegro v Belarus
2000 Macedonia v Bulgaria
2030 Greece v Iceland
2100 Georgia v Kazakhstan
2100 Gibraltar v Latvia
2100 Norway v Finland
2115 Luxembourg v Albania
2130 Austria v Turkey
2130 Sweden v Czech Rep
2130 Switzerland v Bosnia-Herzegovina
2145 Belgium v Portugal
2145 Germany v Italy
2145 R. of Ireland v Slovakia
2200 England v Netherlands
2200 France v Russia
2200 Scotland v Denmark
0 maoni:
Chapisha Maoni