Robo fainali ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho, inatarajiwa kuvurumishwa leo huku vita kubwa ikiwa ni namna ambavyo makocha wawili wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye ni kocha wa Mwadui FC na Selemani Matola ambaye ni kocha wa Geita Gold FC.
Kwa nyakati tofauti makocha hawa waliwahi kuteka vichwa vya habari wakiwa katika benchi la Simba SC. Kinachokumbukwa zaidi kutoka kwa Selemani Matola ni sakata lake na aliyekuwa kocha wa Simba, Dylan Kerr lililopelekea kuondoka kwake Simba SC. Kwa Julio hakuna asiyekumbuka jinsi ya uondokaji wake yeye na Abdallah Kibadeni.
Julio kwa sasa ameichukua Mwadui FC timu inayoonekana kucheza vizuri ikiwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa waliowahi kuwika katika soka la Tanzania. Kubwa kuliko yote Mwadui inaonekana kuwa moja ya timu nzuri licha ya kuwa katika nafasi ya sita ikijikusanyia alama zake 34 kibindoni.
Kwa upande wa kocha Selemani Matola anajivunia kuifikisha timu yake ya Geita Gold na kuwa timu pekee kutoka kwenye madaraja ya chini kufika katika hatua hii.
Mechi hii itatiwa chachu na uwepo wa makocha wawili wanaofahamiana vizuri. Jamhuri Kihwelo na Selemani Matola.
0 maoni:
Chapisha Maoni