Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose
Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atachukua
nafasi ya Louis van Gaal.
Kwa mujibu wa jarida la Don Balonna Mourinho anataka kusajili nyota watatu.
Kocha
huyo ameshaanza mipango ya usajili kwa kuweka wachezaji kadhaa nyota
katika orodha yake akiwemo mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain,
kiungo wa Real Madrid James Rodriguez na mshambuliaji wa Juventus Alvaro
Morata.
Mourinho ameshawahi kufanya kazi na Higuain wakati akiwa
Madrid na United wameonyesha kuwa tayari ingawa watalazimika kulipa
kitita cha paundi milioni 58 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa
kimataifa wa Argentina.
United pia watakabiliwa na upinzani kwa
Morata ingawa Madrid wako tayari kumnunua tena kama mkataba unavyotaka
ili waje kumuuza kwa kiwango cha juu wakati Rodriguez yeye anatarajiwa
kuondoka kiangazi kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.
- Blogger Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni:
Chapisha Maoni