Striker wa Leister City aliingia uwanjani zikiwa zimesalia dakika 20 game kumalizika wakati huo England ikiwa nyuma kwa goli 2-1 dhidi ya Ujerumani, ndani ya dakika tano Vardy akawanyanyua mashabiki kwa kupachika bao.
Goli lake la kwanza kwenye timu ya taifa ya England litabaki kwenye kumbukumbu, beki wa kulia wa Liverpool Nathaniel Clyne alipenyeza krosi ndani ya box kisha Vardy akapachika bao akiunganisha kwa kisigino mpira uliompita golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer.
Takwimu muhimu
- England wamepoteza mchezo mmoja kati ya michezo 18 ya kimataifa iliyopita (W14 D3).
- Harry Kane amefunga goli lake la kwanza baada ya kupangwa kwenye kikosi cha kwanza cha England. Magoli yake matatu yaliyopita yote ameyafunga akitokea benchi.
- England wameshindwa kuzuia kufungwa bao kwenye mechi zao saba zilizopita dhidi ya Ujerumani.
- Ujerumani wamefunga kwa mashuti yao yote yaliyolenga goli (shots on target.)
- Mario Gomez amefunga bao lake la kwanza kwenye timu ya taifa ya Ujerumani tangu June 2012.
- Magoli isa ya yaliyofungwa na wachezaji wa England yote yamefungwa na wachezaji tofauti players (Dier, Vardy, Kane, Rooney, Alli, Oxlade-Chamberlain, Barkley, Sterling na Walcott).
0 maoni:
Chapisha Maoni