
1.CRISTIANO RONALDO
Mshambuliaji huyu hatari ambaye jana ameonesha uwezo wake japo umri umeenda lakini kocha wa Real Madrid, Zidane amekataa katakata kumuuza mchezaji huyo na kutamka kuwa ndiye chaguo lake la kwanza katika kikosi cha timu yake na bado anamhitaji kwahiyo wapinzani mtakula kwa macho Ronaldo hatoki Real Madrid

2.LIONEL MESSI


3.NEYMAR JR
Mshambuliaji mtoto ambaye anazidi kung'ara katika timu ya Barcelona na Brazil kutokana na kiwango chake.Yeye ndiye anaonekana kuja kuwa mrithi rasmi wa mshambuliaji Lionel Messi hivyo klabu hiyo kubwa ya hispania haitakuwa tayari kumrusu kijana huyo kuihama timu yake ya Barcelona kwahiyo timu pinzani mtakula kwa macho

pia dogo huyu ana mabao 21 katika ligi kuu ya hispania maarufu kama La Liga chini ya Karim Benzema wa Real Madrid
4.ROBERT LEWANDOSKI
Mshambuliaji hatari wa Bayern Munchen ambaye anazidi kutakata katika ligi ya Ujerumani kwa sasa haitowezekana kuihama timu hiyo kutokana na umuhimu wake katika timu hiyo ya Bundesliga kwani hata kama kocha wa timu hiyo akihama kwenda Manchester City yeye atabaki pale na amesema kwamba ana furahia maisha yake ya klabuni hapo na klabu nyingine zimuache kwanza kwani hayupo tayari kuihama klabu hiyo

5.DAVID DE GEA
Kipa muhimu katika kikosi cha mashetani wekundu ambaye ameweza kuonyesha uwezo alionao kwa kupanguamichomo hatari ya washambuliaji mbalimbali na kuthibitisha kwamba yeye ni bora katika kikosi hicho.

Aliwahi kutakiwa na klabu ya Real Madrid katika msimu uliopita lakini walimkosa baada ya kushindwa kubadilishana kipa huyo na beki Sergio Ramos kwahiyo aliongeza mkataba na hatoweza kuhama timu hiyo kwa wakati huu
0 maoni:
Chapisha Maoni