Mkufunzi wa Aston Villa aondoka baada ya siku 147


Mkufunzi wa kilabu ya Aston Villa Remi Garde ameondoka katika kilabu hiyo kupitia maelewano baada ya kuhudumu kwa siku 147 katika kilabu hiyo iliopo katika mkia wa jedwali la ligi ya Uingereza.
Remi Garde mwenye umri wa miaka 49 alichukua pahali pake Tim Sherwood katika kandarasi ya miaka mitatu na nusu ,lakini anaondoka baada ya kushindwa mara sita mfululizo.
Mechi yake ya mwisho ilikuwa kushindwa kwa 1-0 dhidi ya Swansea mnamo tarehe 19 mwezi Machi ,matokeo yalioiwacha Villa pointi 12 ikiwa katika hatari ya kushushwa daraja.
Villa ilishinda mechi mbili kati ya 20 wakati wa uongozi wa Garde.
Taarifa ya kilabu ilimshukuru mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal kwa juhudi zake wakati wa kipindi kigumu na kusema Erick Black atachukua pahali pake kwa mda.
Uamuzi huo wa kuwachana na Garde unafuatia siku nane za majadiliano ambayo yalikamilika siku ya Jumanne.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni