Imegundulika
kwamba kampuni kubwa la utengenezaji mavazi michezoni , Adidas,
linatarajia kusitisha mkataba wa mamilioni ya dola kwa bodi ya
wanariadha ulimwenguni kufuatia kashfa zinazowakumba wanariadha za
utumizi wa dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Mkataba huo baina ya
ADIDAS uliodumu kwa muda wa miaka kumi na mmoja na shirikisho la
wanariadha la kimataifa ulikuwa uendelee mpaka kufikia mwaka 2019.
Lakini imefahamika kwamba Adidas imeamua kusitisha mkataba huo miaka
mitatu kabla ya wakati, kufuatia matokeo ya kashfa hizo za moja kwa
moja.Hatua hiyo inafuatia shirikisho hilo la riadha ulimwenguni limegubikwa na madai hayo wa hali iliyofadhiliwa na Urusi.
Ufadhili wa vifaa hivyo vya michezo kwa IAAF unakadiriwa kufikia thamani ya dola za kimarekani milioni thelathini na tatu. Hata hivyo si Adidas ama IAAF walioweza kuzungumzia suala hili katika hatua za awali.
0 maoni:
Chapisha Maoni