Akaunti ya Tiffah yasoma Sh.Mil 200



d



Dar es Salaam: Watoto ni Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu! Wakati akitimiza siku 180 yaani nusu mwaka tangu kuzaliwa mwezi Agosti mwaka jana, imebainika kwamba akaunti ya benki ya mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’ inasoma zaidi ya Sh. Milioni 200,

TIFFAH AFUNGULIWA AKAUNTI
Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa familia ya Diamond na mzazi mwenzake, Zarinnah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ zilieleza kwamba, Tiffah almaarufu Tiffah Dangote alifunguliwa akaunti ya watoto kwenye benki maarufu Bongo ambapo jamaa huyo alianza kwa kumwingizia Sh. Milioni 10.
Chanzo hicho kilidadavua kwamba, wakati wa kumtoa mtoto huyo kwenye ile sherehe ya 40 ya Tiffah iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, akaunti hiyo ilianza kunona baada ya kuingizwa Sh. milioni 40 zilizotolewa na wadhamini wa shughuli hiyo ambao walikuwa ni makampuni tofauti ikiwemo bendi moja.

DIAMOND AMWEKEA MIL. 10 KILA MWEZI
Imefahamika kwamba, Diamond amekuwa akiingiza Sh. milioni 10 kwenye Akaunti ya Tiffah kila mwezi hivyo kwa miezi sita ni jumla ya Sh. milioni 60.
Inasemekana kwamba, kwa sasa Diamond ana furaha isiyo kifani baada ya wikiendi iliyopita kulamba dili la Tiffah la matangazo na kampuni moja kubwa ya huduma za simu nchini.

DILI LA MIL. 50
Ilielezwa kwamba mkataba huo wa mwaka mmoja ndiyo dili kubwa zaidi kwa mtoto huyo katika madili yote ukieleza kukaribia Sh. milioni 50.
11327388_130237883993111_1598321086_nMbali na mkataba huo, pia kuna dili nyingine mpya ya pampers za watoto zenye jina la Tiffah ambazo zitaanza kusambazwa nchi nzima na kampuni ambayo nayo imemmwagia Tiffah ‘mpunga’ wa maana huku akila mashavu mengine kwenye makampuni ya mama yake nchini Afrika Kusini na Uganda.

MADILI YOTE MIL. 200
“Wale jamaa wa pampers wameingia naye mkataba siyo chini ya Sh. Milioni 50 hivyo ukichanganya madili yote akaunti ya Tiffah ina mshiko mrefu si chini ya Sh. milioni 200,” chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu huku kikiweka wazi kuwa hata Diamond mwenyewe amekuwa akidai kuwa kuna mastaa wakubwa Bongo lakini wanafunikwa na Tiffah kwa mkwanja.

MBALI NA FEDHA TASLIMU
Imeelezwa kwamba, mbali na fedha taslimu, katika kipindi hicho cha miezi sita, Tiffah amekuwa akigombewa ili awe balozi wa maduka ya nguo na shule za watoto huku baadhi ya maduka yakimruhusu kufanyiwa ‘shopping’ bure kwenye maduka hayo huku shule zikiahidi kumsomesha bure atakapofikisha umri wa kuanza kusoma.
“Unajua kitendo cha Tiffah kujulikana kuwa amefanyiwa shopping kwenye duka lako, tayari utakuwa umejitangaza sana. Ndivyo wanavyoamini watu wa biashara na masoko.
zari1“Vivyo hivyo kwa upande wa shule, wanaamini kuwa ikijukana Tiffah ni balozi wa shule fulani basi wazazi watapenda kupeleka watoto wao kwenye shule husika maana watoto wao nao watakuwa na nafasi ya kumuona Tiffah ambaye kwa sasa ni staa mkubwa,” kilifunguka chanzo hicho.

DIAMOND AANIKA MKATABA MPYA
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, gazeti hili lilimtafuta Diamond au Dangote ili kufungukia madili ya Tiffah ambayo hadi sasa ameshalamba na kumfanya kuwa na kiasi hicho cha fedha ambapo alifunguka:

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa mtoto mzuri, Tiffah Dangote, achana na maneno ya watu juu yake lakini ukweli ni kwamba hata hiyo milioni 200 uliyotajiwa ni kidogo.
“Kuna mkataba mwingine mnono sana amepata na kuna vitu vingine vikubwa vinakuja kwa Tiffah. Ukweli sasa hivi nimeamini watoto ni neema tupu,” alisema Diamond akimuomba mwandishi wetu kuwaambia Watanzania kuwa Tiffah aliyezaliwa Agosti 6, 2015 ni mali yake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni