Muimbaji maarufu wa
muziki wa kizazi kipya Chris Brown ameondolewa lawama yawizi na
kupigana na utawala wa Las Vegas Marekani baada ya mwanamke mmoja kudai
alimzaba kofi na kumpokonya simu yake walipokutana kwenye Kasino moja
ya kamari mapema mwezi huu.
Mkuu wa sheria katika jimbo hilo Steve
Wolfson amesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia msanii
huyo mashtaka ya utovu wa nidhamu kwa kumshambulia mwanamke huyo na
kumuibia simu .- Polisi walikuwa wameandikisha ripoti iliyodai kuwa Brown alimpiga mwanamke mmoja na kumpokonya simu yake alipojaribu kumpiga picha akijivinjari katika sherehe moja ya kibinafsi.
Mwaka 2009, Brown aliagizwa kukaa miaka mitano bila kufanya kosa lolote baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga nyota wa muziki wa pop Rihanna.
0 maoni:
Chapisha Maoni