Novak Djokovic amefuzu kwa fainali ya mashindano ya tenisi ya Australian Open kwa mara ya sita baada ya kumbwaga Roger Federer.
Mchezaji huyo nambari moja duniani amepata ushindi wa 6-1 6-2 3-6 6-3.Djokovic alitawala seti mbili za kwanza, lakini baada ya muda Federer alianza kujikwamua.
Hata hivyo, Djokovic alifanikiwa kushinda seti ya mwisho.
Hili ni shindano la tatu mtawalia la Grand Slam ambapo Djokovic amemshinda Mswizi huyo ambaye sasa atasubiri kwa muda zaidi kushinda taji lake kuu la 18.
Djokovic atakutana na Mwingereza Andy Murray au raia wa Canada Milos Raonic kwenye fainali.
Mserbia huyo amemshinda Murray kwenye fainali mara tatu awali, ikiwa ni pamoja na mwaka jana aliposhinda kwa seti nne.
"Nilicheza vyema sana seti mbili za kwanza lakini ilinibidi kwa sababu Roger amekuwa akicheza vyema sana na nilijua angekuwa mkali,” amesema Djokovic baada ya ushindi wa leo.
0 maoni:
Chapisha Maoni