Pato: Chelsea ndio makao yangu mapya

 
Pato alijiunga na AC Milan mwaka wa 2007 akiwa na umri wa miaka 17. 

 
Mshambulizi wa Corinthians Alexandre Pato amesema kuwa Chelsea ndio makao yake mapya.
Pato aliyasema hayo huku dukuduku zikisema kuwa huenda anaelekea Stamford Bridge kwa mkopo.
Mshambulizi huyo wa zamani wa AC Milan, 26, aliwasili Uingereza jumatano usiku kwa majaribio kabla ya kutia sahihi mkataba wa muda hadi m,ei.
Chelsea haijasema lolote kuhusu habari hizo zinazomshirikisha Pato, ambaye amekuwa nchini Brazil kwa mkopo kwa misimu miwili.
"Natamani sana kuichezea Chelsea. Nahitaji kucheza. nafurahia sana uhamisho huu.'' alisema Pato.
Pato alijiunga na Milan mwaka wa 2007 akiwa na umri wa miaka 17.
Hata hivyo hakushamiri kama ilivyotarajiwa na ikambidi kurejea Brazil mwaka wa 2013.
Tayari amefunga mabao 10 katika mechi 25 alizoichezea Brazil, ijapokuwa mara ya mwisho alipoitwa katika kikosi cha taifa ilikuwa ni 2013.
 
 
Pato ameingia Chelsea wakati ambao kiungo wa Chelsea Ramires amejiunga na Jiangsu Suningin ya China
Vilevile alishinda nishani ya fedha katika michezo ya olimpiki ya London mwaka wa 2012.
''Nawashukuru sana mashabiki wa Chelsea kwa imani waliokuwa nayo kwangu ''Ningependa kuwajua wachezaji wenzangu wapya na pia kupata marafiki wap-ya huko Stamford Bridge.
Pato ameingia Chelsea wakati ambao kiungo wa Chelsea Ramires amejiunga na Jiangsu Suningin ya China kwa gharama ya pauni milioni £25m.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni