Timu ya Kenya ya
mchezo wa voliboli itakayoshiriki kwenye mashindano ya kufuzu kwa
Michezo ya Olimpiki imelalamikia maandalizi duni.
Kocha mkuu wa
timu ya taifa ya Kenya ya wanawake ya voliboli, Japheth Munala,
amesikitishwa na serikali kutoisaidia timu hiyo licha ya kwamba
inasafiri Yaounde, Cameroon, kuiwakilisha Kenya katika mashindano hayo
ya kufuzu.“Tumekua mazoezini tangu mwezi Disemba mwaka jana na mpaka sasa hakuna afisa yoyote wa serikali ametutembelea,'' asema Munalo.
“Inasikitisha sana sisi twatoa jasho hapa lakini hamna yoyote anayetilia maanani maslahi yetu. Hata marupurupu hatujapata tofauti na mataifa kama Misri yanayopewa motisha wa kutosha na serikali yao.''
Mashindano hayo ya kufuzu kwa michezo ya Olympiki yatafanyika Yaounde, Cameroon, kuanzia tarehe 12-19 mwezi ujao.
Timu hiyo imo mazoezini ukumbi wa Kasarani mjini Nairobi.
Kenya ni baadhi ya mataifa 17 yatakayoshiriki mashindano hayo. Mshindi ataiwakilisha Afrika katika michezo ya Olympiki mjini Rio de Janeiro, Brazil mwezi Agosti mwaka huu.
Mbali na Kenya miongoni mwa mataifa 17 yatakayoshiriki kwa mashindano ya kufuzu ni wenyeji Cameroon, Algeria, Tunisia, Nigeria, Botswana, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda, Misri na Uganda
0 maoni:
Chapisha Maoni