Ijumaa
Usiku Manchester United watafungua michuano ya Raundi ya 4 ya EMIRATES
FA CUP kwa kucheza Ugenini huko Pride Park Stadium na Timu ya Daraja la
chini la Championship, Derby County, huku wakitokea kwenye kipigo chao
cha kwanza cha Mwaka 2016 mikononi mwa Southampton.
Derby wao wapo
Nafasi ya 6 kwenye Msimamo wa Ligi ya Championship lakini hawajashinda
katika Mechi zao 5 zilizopita za Ligi na Jumatatu iliyopita walitandikwa
4-1 Ugenini na Burnley.
Derby ipo chini ya Meneja Paul Clement ambae alikuwa Msaidizi wa Carlo Ancelotti walipokuwa Chelsea na Real Madrid.
Uso kwa Uso
Hii
itakuwa Mechi ya 104 kati ya Derby na Man United huku Vigogo hao wa
Ligi Kuu England wakishinda Mechi nyingi na ya mwisho ilikuwa 4-1 kwenye
Raundi ya 6 ya FA CUP Msimu wa 2008/09.
Mara ya mwisho kwa Derby kuifunga Man United ilikuwa ni 1-0 kwenye Kombe la Ligi Mwezi Januari 2008.
Hali za Timu
Man
United huenda ikamkosa Matteo Darmian ambae aliumia kwenye Mechi yao ya
mwisho dhidi ya Southampton huku kukiwa bado hamna uthibitisho kama
Majeruhi Phil Jones, Marcos Rojo, Michael Carrick na Bastian
Schweinsteiger wako fiti kwa Mechi hii lakini Ashley Young, Antonio
Valencia na Luke Shaw atakuwa nje kwa vile ni Majeruhi wa muda mrefu.
Derby
wao wana Kikosi kamili na Wachezaji wao hatari ni Straika Nick Blackman
akijumuika na Mastraika wa zamani wa Aston Villa, Darren Bent na
Andreas Weimann, pamoja na Chris Martin. REFA: Anthony Taylor
EMIRATES FA CUP
Raundi ya 4
Ijumaa Januari 29
22:55 Derby v Man United
Jumamosi Januari 30
15:45 Colchester v Tottenham
Zote kuanza Saa 12 Jioni
Arsenal v Burnley
Crystal Palace v Stoke
Nottm Forest v Watford
Oxford Utd v Blackburn
Shrewsbury v Sheff Wed
Portsmouth v Bournemouth
Aston Villa v Man City
Reading v Walsall
Bolton v Leeds
West Brom v Peterborough
Bury v Hull
20:30 Liverpool v West Ham
Jumapili Januari 31
16:30 Carlisle v Everton
19:00 MK Dons v Chelsea
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016
Home / FOOTBALL /
SPORTS
/ EMIRATES FA CUP: IJUMAA NI DERBY vs MANCHESTER UNITED PRIDE PARK! REFA NI ANTHONY TAYLOR
- Blogger Comment
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni:
Chapisha Maoni