GERVINHO AIHAMA AS ROMA

Gervinho-Hebei
Klabu ya AS Roma imetangaza rasmi kumuuza mchezaji wake Gervinho kwenda Hebei China Fortune FC kwa ada ya €18m pamoja na bonus ya €1m.
Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast jana alipigwa picha akiwa ameshikilia jezi ya klabu yake mpya ambayo ataitumikia lakini mambo mengine ya kimkataba yamefanyika leo.
“Leo AS Roma inaweza ikathibitisha kwamba mshambuliaji wake Gervinho amejiunga na Hebei China Fortune FC,” ilisomeka sentensi hiyo.
“Muaivory Coast huyo mwenye miaka 28 amesaini mkatba na klabu hiyo ya China kwa mkataba wa kudumu wenye thamani ya €18 million baada ya kudumu na AS Roma kwa misimu miwili na nusu”.
“Nyongeza ya €1 million italipwa kutegemea na kiwango cha mchezaji huyo kwenye klabu hiyo ya China”.
Gervinho alijiunga na Roma majira ya joto ya mwaka 2013 akitokea Arsenal na kucheza mchezo wake wa kwanza wa mashindano August 203 dhidi ya Livorno ambapo Roma iliibuka na ushindi wa bao 2-0.
Alifunga goli lake la kwanza kwenye ligi ya Serie A akiwa Roma kwenye ligi ya akicheza mchezo wa pili kwenye klabu hiyo dhidi ya Sampdoria mchezo uliomalizika Roma wakiwa washindi kwa bao 2-0.
Gervinho amecheza michezo 88 kwenye mashindano yote akiwa anaitumikia Roma na kufunga magoli 26. Amefunga magoli saba kwenye mechi 17 msimu huu.
Mechi yake ya mwisho akiwa Roma ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Milan mchezo uliochezwa January 9, 2016.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni