Branislav Ivanovic.
Mashabiki wa Chelsea popote duniani watakuwa na furaha baadaya beki wa klabu hiyo, Branislav Ivanovic kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye makazi yake London, Uingereza.
Mkataba wa awali wa Ivanovic ulikuwa ukimalizika mwishoni kwa msimu huu na baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja anataraji kuendelea kuichezea Chelsea mpaka mwishoni kwa msimu wa 2017.
Kabla ya kuongeza mkataba na Chelsea tayari kuna baadhi ya klabi zilikuwa zimeanza kuonyesha nia ya kuhitaji kumsajili beki huyo ambapo baadhi ya klabu hizo ni AC Milan na Inter Milan ambazo zote zilikuwa zimeanza kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo.
Ivanovic alisajiliwa na Chelsea mwaka Januari 2008 akitokea klabu ya Lokomotiv Moscow na ameshaichezea michezo 341 na kufunga magoli 32 huku akiwa ameshinda mataji mawili ya ligi kuu ya Uingereza, Kombe la FA mara nne, Kombe la Capital One mara moja na Kombe la Europe na ligi ya mabingwa Ulaya yote mara moja moja.
0 maoni:
Chapisha Maoni