Pep Guardiola.
Baada ya wiki kadhaa kupita tangu kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kuweka wazi mipango yake kuwa anapendelea kwenda kufundisha soka Uingereza imefahamika kuwa anafanya mazungumzo na moja ya klabu kubwa ya Uingereza.
Gazeti la Ufaransa la L’Equipe limeripoti kuwa kocha Guardiola alionekana wiki iliyopita katika hotel ya Bristol iliyopo jijini Paris akifanya mazungumzo na baadhi ya maafisa kutoka Manchester United ambao walikuwa wakifanya mazungumzo.
Baada ya taarifa hiyo kusambaa katika sehemu mbalimbali ni wazi kuwa Manchester United itakuwa imeshinda wapinzani wao Manchester City na Chelsea ambao nao walikuwa wakionyesha nia ya kumtaka kocha huyo wa zamani wa Barcelona.
0 maoni:
Chapisha Maoni