Mabondia
Georger Dimoso (kushoto) wakitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati
wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa
Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe
Ndava.(Picha na SUPER D BOXING NEWS).
MABONDIA Abdallah Pazzi na Georger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74.
Akizungumza
wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif
amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi
wa mkoa wa pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo.
Aliongeza
kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya
udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na
ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi
mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini.
“Bagamoyo
hatuna jukwaa ‘ring’ la ngumi hata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es
salaam yaje hapa ndio vijana wapate kucheza. “Hivyo naomba wadau
mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hilo ili mchezo
wa ngumi usonge mbele hapa” alisema
Siku
hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na
shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito
wa kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa
kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba
atakumbana na Twalibu Tuwa.
Katika
mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo
wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali
kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia
kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu
Mhamila ‘Super D’ kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine
kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha.
0 maoni:
Chapisha Maoni