Waandalizi wa Tuzo
za Oscar wameahidi kuwa wataimarisha juhudi zao za kuongeza wanachama
zaidi wanawake na watu wa kutoka katika jamii za wachache kama vile watu
weusi ifikapo mwaka 2020.
Marekebisho yamefanywa baada ya juma
moja la lawama baada ya kukosa washindi weusi walioorodheshwa kutangazwa
katika hafla ya shughuli hizo mwezi ujao.Haki ya upigaji kura kwa wanachama pia imewekewa muda wa miaka kumi pekee.
Waigizaji na waandalizi kadha wa filamu kama vile mwigizaji Will Smith na mwandalizi mkuu Spike Lee wamesema kuwa watasusia hafla za tuzo za Oscar mwaka huu kwa kuwa wote walioteuliwa ni wazungu.
0 maoni:
Chapisha Maoni