NEYMAR AIBEBA BARCELONA BILA MESSI NA SUAREZ

Neymar JR
Neymar amekiongoza kikosi cha Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Copa del Rey wakiwa ugenini kwenye dimba la San Mames Stadium.
Neymar Jr 3
Barcelona ambao ndiyo mabingwa watetezi walishuka uwanjani bila nyota wao wawili Lionel Messi pamoja na Luis Suarez wanaokamilisha combination ya ushambuliaji iliyopewa jina la MSN ambayo inaundwa na Messi, Suarez pamoja na Neymar na kutajwa kuwa safu hatari ya ushabuliaji duniani kwa sasa.
Neymar Jr 1
Barcelona walipata magoli yao mawili ndani ya dakika 25 za kipindi cha kwanza. Goli la kwanza lilifungwa na Munir el Haddadi dakika ya 18 kwa kuunganisha krosi ya Ivan Rakitic kabla ya Neymar kupasia kamba dakika ya 24 na kuiandikia Barcelona bao la pili lililoipa timu yake ushindi.
Neymar Jr 2
Aritz Aduriz aliipatia Bilbao bao la kufutia machozi dakika ya 89 na timu hizo zitakutana tena kwenye mchezo wa marudiano Jumatano ya juma lijalo.
Vikosi vilivyoanza vya timu zote mbili pamoja na wale walionzanzia benchi na wachezaji waliooneshwa kadi za njano viko hapa chini:
Barcelona vs Bilbao
Takwimu za mchezo kati ya Celta Vigo vs Barcelona zilikuwa kama ifuatavyo:
Barcelona vs Blbao 1
Mchezo mwingine wa mashindano hayo umeishuhuia Atletico Madrid ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Celta Vigo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni