BAADA YA KUVUNJA MKABA NA INTER MILAN, KLABU YA EPL YAMFUKUZIA NEMANJA VIDIC

Nemanja
Klabu ya Aston Villa ya England imetoa offer kwa Nemanja Vidic kumsaini kama mchezaji huru baada ya nyota huyo wa zamani wa Manchester United kuvunja mkataba na klabu yake ya Inter Milan inayoshiriki ligi kuu ya soka ya Serie A nchini Italia.
Vidic, 34, anahusishwa kutimkia kucheza soka nchini Marekani kwenye ligi ya MLS lakini pia huenda akarejea nchini England kukipiga kwenye Premier League.
Nemanja 1
Aston Villa wamekuwa wakipambana kusaka kiongozi atakayeiongoza safu yao ya ulinzi, mbali na Vidc Villa wanaifukuzia pia saini ya mlinzi wa kati wa Bordeaux Lamine Sane.
Joe Lescott huenda akatimkia China huku pia kukiwa na taarifa beki huyo wa zamani wa Man City anaweza akajiunga na klabu ya LA Galaxy ya Marekani.
Mserbia Nemanja Vidic ameiacha klabu ya soka ya Inter Milan ya nchini Italia baada ya mkataba wake kusitishwa kwa makubaliano maalumu, klabu ya Italia alisema Jumatatu.
Nemanja 2
Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United alijiunga na klabu hiyo ya Inter Millan mwezi Julai 2014 na kuichezea mechi 28 tu katika msimu wa mwaka jana, lakini akashindwa kucheza tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kutingwa na majeruhi.
“Klabu ya Internazionale wangependa kutangaza kwamba klabu inavunja mkataba na Nemanja Vidic baada ya maridhiano maalumu”, Inter iliandika katika tovuti yake.
Nemanja 3
Vidic, ambaye pamoja na mlinzi mwenzie Rio Ferdinand walitengeneza ngome isiyo na kifani nchini England na Ulaya kwa ujumla, na kuisaidia klabu ya Manchester United kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo pia Ligi ya Mabingwa ulaya mwaka 2008, ameishukuru klabu ya Inter na mashabiki wake, “Napenda kuwatakia mafanikio makubwa zaidi kama klabu katika siku zijazo” alimalizia Vidic.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni