
- Paul Dybala $68.28m
Haishangazi
kumuona kinda huyu mwenye kipaji katika orodha ya wachezaji 20 wenye
thamani kubwa zaidi hivi sasa, Juventus inajivunia kijana huyu na hawapo
tayari kumuuza hivi sasa kutokana na uwezo wake wa kucheza sehemu
yeyote katika mstari wa mbele wa ushambulizi.
- Diego Costa $71.56m
Mshambuliaji
huyu wa Chelsea amekua hana msimu mzuri tangu kuanza kwa msimu huu
lakini fomu yake ya mwaka jana inamfanya aingie katika orodha hii ya
wachezaji 20 wenye thamani kubwa.
- Romelu Lukaku $74.51m
Inakupa
maswali mengi kwanini kocha Jose Mourinho alimuachia kijana huyu raia
wa Ubelgiji mwenye miaka 22. Lukaku ameendelea kuzifumania nyavu akiwa
na klabu ya Everton na hivi sasa anaongoza katika kinyang’anyiro cha
ufungaji mabao nchini England.
- Gareth Bale $75.49m
Majeruhi
yanayomuandama mchezaji huyu huenda yamechangia kuwa pamoja na kuwa
ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa gharama kubwa zaidi duniani, lakini
thamani yake imepungua sana hadi sasa anashika nafasi ya 17. Anahitaji
kupandisha gemu yake huku akibakia free injury ili arudi katika ubora
wake.
- Robert Lewandowski $76.03m
Rekodi
yake ya mabao akiwa na Bayern Munich msimu huu na uliopita unamfanya
Mpoland huyu kuwa mshambuliaji hatari zaidi wa kati duniani.
- Thomas Muller $77.89m
Huyu
ni pacha wa Robert Lewandowski katika safu ya ushambuliaji, rekodi zake
za mabao akiwa Bayern na timu ya taifa ya Ujerumani inamfanya Muller
kuwemo katika orodha hii.
Huyu
bila shaka ni mchezaji Liverpool wanajivunia zaidi kuwepo katika kikosi
chao hivi sasa. Amekua akifunga mabao muhimu sana, Liverpool wanahitaji
kumshikiria mchezaji huyu kwani anaweza kushawishika kuihama klabu hiyo
siku za usoni.- Kevin de Bruyne $79.75m
Kama
ilivyo kwa Mbrazil Philippe Coutinho, Kevin de Bruyne ni moja ya
wachezaji hatari zaidi katika mstari wa pili nyuma ya mshabuliaji.
Haikua kazi kwa Manchester City kuilipa Wolfsburg pauni 54m kumnasa
mbelgiji huyu.
- Paul Pogba 84.45m
Kiungo
huyu wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, alitajwa katika kikosi
cha wachezaji 11 bora duniani pamoja na akina Lionel Messi na Cristiano
Ronaldo, ni miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo wanaozivutia klabu
nyingi sana hivi sasa.

Usajili wake kujiunga na Manchester United tena kwa pesa nyingi zaidi akiwa na umri wa miaka 19 tu, ulitajwa na wengi kama kamali, kijana huyu hivi sasa, pamoja na United kutokua na msimu mzuri, Martial anaonesha kuwa msaada mkubwa Old Trafford.
- Alexis Sanchez $89.47m
Huwezi
kuwataja wachezaji watatu muhimu zaidi katika kikosi cha Arsenal
ukamuacha Alexis Sanchez. Raia huyu wa Chile anastahili kuwa katika
orodha hii.
- Sergio Aguero $89.69m
Anaweza
kuwa ndiye mchezaji bora zaidi wa muda wote wa klabu ya Manchester
City, ana kila kitu mshambuliaji anastahili kuwa nacho.
- Luis Suarez $94.28m
Umoja
wake na Lionel Messi, pamoja na Neymar katika kikosi cha Fc Barcelona,
unamfanya Suarez kuwa miongoni mwa wachezaji wenye thamani kubwa zaidi
hivi sasa.
- Antoine Griezmann $96.46m
Baada
ya kuondoka kwa mastaa kadhaa kikosini Atletico Madrid, Mfaransa huyu
anabakia kuwa tegemezi zaidi huku akifunga magoli karibu kila mechi.
- Raheem Sterling $98.10m
Ugumu wa usajili wake kutoka Liverpool, sanjari na pesa waliyoitoa Manchester City unaonesha thamani halisi ya Raheem.
- Harry Kane $99.74m
Ukitaka
kujua thamani halisi ya kijana huyu mwingereza, ni pale utakapoamua
kutaka kumsajili, ana kila kitu mshambuliaji anatakiwa kuwa nacho.
- Cristiano Ronaldo $124.54m
Amemaliza kila kitu, umri unasogea, moja kati ya wachezaji bora zaidi kuibariki dunia ya mpira.
- Eden Hazard $142.56m
Wengi
tunaweza kushtushwa na jina la Hazard katika nafasi ya tatu, lakini
tukumbuke kuwa thamani ya mchezaji inahusisha vitu vingi sanjari na
uwezo uwanjani, lakini pia mauzo ya jezi n.k


0 maoni:
Chapisha Maoni