SADIQ MOMBA NA BAINA MAZOLA KUZIPIGA TASUBA BAGAMOYO





MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola wamesaini mkataba wa kupigana Machi 5,  katika Ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani
Akizungumza na gazeti hili, promota wa pambano hilo Muhsin Sharif alisema pambano hilo ni la uzani wa kg 59, na litakuwa la raundi nane.
“Nimeamua kuwapambanisha mabondia hawa kwani ndio wanatamba kwenye uzito huo kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini”, alisema Sharif

Pia Sharif alisema Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa akifanya vizuri awape nje hata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand alipigwa kwa KO ya raundi ya tatu hivyo anahitaji ushindi na pointi za kutosha kumrudisha kileleni.


Kwa upande wa Mazola katika uzito wake yeye  ni namba tatu katika ngumi hapa nchini hivyo anataka kuwa zaidi ya bondia Momba

Wadadisi wa ngumi wanasema Momba baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi wadogo zake wamepania kucheza nae kwani inaonekana kiwango chake kimepungua.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni