Shilole live na kidume mpya



IMG-20160122-WA0014
Staa mwenye makeke wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake mpya.
Stori: Imelda Mtema, Wikienda
Dar es Salaam: Baada ya kumwagana na aliyekuwa mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, staa mwenye makeke wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametua kwa kidume mpya ambaye ndiye mrithi wa Nuh ambapo wikienda iliyopita alijiachia naye ‘live’ wakiwa nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
12345877_995909120472037_551476580_nAkizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu wikiendi iliyopita, Shilole alifunguka kwamba hataki tena ‘stresi’ kama alizokuwa akizipata kwa mpenzi wake huyo wa zamani hivyo sasa hivi anataka maisha ya furaha na jinsi gani ya kutumia akili yake ili kutengeneza fedha.
“Acha tu sasa hivi nipunguze machungu yangu maana sihitaji tena stresi, nimepumzisha akili yangu kwa mtu sahihi kabisa ambaye nafikiri yuko karibu yangu, mambo ya Nuh tupa kule,” alisema Shilole au Shishi.
Msanii huyo alifunguka kuwa maisha yake yamebadilika kabisa na hataki kuwa na kitu cha historia ambacho kilimuumiza na kumtesa kwani anataka maisha mapya kabisa ndiyo maana ameamua kutumbua majipu ambayo yalikuwa yakimsumbua.
Kwa upande wake Nuh alipotafutwa kujua mtazamo wake baada ya Shishi kumwanika mwanaume wake mpya, jamaa huyo hakuwa na la kusema zaidi ya kumtakia Shilole kila la heri.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni