BAADA YA SIMBA KUPIGA MTU ‘MKONO’, HUU NDIYO ULIKUWA UJUMBE WA MWINYI KAZIMOTO

Mwinyi Kazimoto 1
February 3 Simba ilitoa kipigo kikali cha magoli 5-1 dhidi ya Mgambo JKT na kutengeneza mazingira mazuri ya kuwania ubingwa msimu huu baada ya kufikisha poini 39 sawa na Azam huku ikiwa pointi moja nyuma ya vinara wa ligi Yanga SC.
Tuachane na matokeo ya Simba na Yanga, lengo langu hapa ni kukufikishia ujumbe ambao ameuandika kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto kupitia account yake ya facebook mara baada ya mchezo wa Simba vs Mgambo JKT kumalizika.
Mwinyi ame-post ujumbe kwenye account yake ya facebook unaosomeka kama ifuatavyo: “asanteni kwa kuja,,,tanx 4 coming, coming, coming in MwanaFA voice ,,,,kesho safari ya kuelekea shinyanga asante MUNGU kwa yote kwa point 3 za leo,,ya leo yamepita tuangalie yajayo ya shinyanga,,..via sindano za sumu#..NGUVU MOJA”.
Kwenye mchezo wa leo, Kazimoto alifunga bao moja kwa shuti kali kati ya magoli hayo matano yaliyofungwa kwenye mchezo huo.
Lakini kabla ya mchezo huo, Kazimoto aliandika pia kwenye account yake ya facebook ujumbe ambao ulikuwa unasomeka kwa maneno haya: “mzunguko wa pili unakuwaga mgumu coz kila timu inapambana kushinda hili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuwa mabingwa ama kuepuka kushuka daraja kwa io kila mchezo ni mgumu kwa kipindi hiki”.
“Kutokana na maandalizi na molali ya team yetu na hakika tutafanya vizuri naomba tu support team yetu kila wakati na hakika badae tutakua pamoja taifa kwa uwezo wa muumba tutafka salama taifa tukapambane tuchukue point 3 muhimu leo japo mchezo utakua mgumu…..via sindano za sumu# kimya kimya#red army#..NGUVU MOJA..”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni