Mechi ya Serie A kati ya Lazio dhidi ya Napoli iliahirishwa baada ya kutokea vitendo vya ubaguzi wa rangi vlivyokuwa vikifanywa na mashabiki wa Lazio kwa beki wa kati wa Napoli half Kalidou Koulibaly.
Ripoti kutoka kwenye mchezo mchezo huo zinasema kwamba, kelele kumfananisha beki huyo na nyani zilikuwa zikipigwa na mashabiki wa Lazio kutoka kwenye majukwaa zilizopelekea mwamuzi kuumaliza mchezo huo uliokuwa umefika dakika ya 68 huku Napoli ikiwa mbele kwa bao 2-0.
Lazio wanaweza wakakumbana na adhabu kubwa ya fine kutokana na tabia iliyofanywa na mashabiki wake.
Boss wa Napoli Maurizio Sarri amempongeza mwamuzi wa mchezo huo Massimiliano Irrati kwa kuusimamisha mchezo kisha asema anajisikia vibaya kusikia kelele za kibaguzi kwenda kwa Koulibaly.
Gonzalo Higuan na Jose Callejon walishaweka kambani na kuendelea kuiweka timu yao kileleni mwa Serie A pointi mbili mbele ya Juventus wakati wazee wa kubagua Lazio wao wakiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi.
0 maoni:
Chapisha Maoni