Baba mzazi wa Isha Mashauzi kuzikwa leo Dar


ISHA
Picha ndogo ni baba yake Isha Mashauzi mwenye kipaza sauti.
BABA mzazi wa mwimbaji Isha Mashauzi, Ramadhan Makongo,  aliyefariki Jumamosi alfajiri wiki iliyopita, anazikwa leo (Jumatatu) saa 6 mchana huko Mbezi kwa Musuguri, jijini Dar es Salaam kwenye makaburi ya Msingwa.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Msuguri ambapo shughuli yote itafanyika ikiwa pamoja na kisomo, sadaka ya chakula  na kumswalia marehemu kabla ya kwenda kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele.
Mtoto wa marehemu, Juma Ramadhan,   amesema  hiyo ndiyo taarifa rasmi na sahihi baada ya kuwepo vuguvugu la sintofahamu juu ya wapi baba yake angezikwa kati ya Dar es Salaam na Musoma. Ramadhan Makongo ambaye pia ni baba wa mwimbaji wa taarab Saida Ramadhan na mume wa mwimbaji Rukia Juma, alifariki katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa siku kadhaa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni