SUAREZ: NATAMANI SIKUMOJA NIREJEE TENA LIVERPOOL

Carragher
Jamie Carragher amesafiri hadi Barcelona wiki iliyopita kwa ajili ya kufanya mazungumzo maalumu na mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool Luis Suarez.
Suarez ameelezea namna alivyoweza kuendana na mfumo wa Barcelona pamoja na ndoto zake za kuhakikisha wanatetea ubingwa wa Champions League na namna ilivyokuwa rahisi kucheza sambamba na Messi na Neymar.
Licha ya uondokaji wake katika kikosi cha Liverpool, Suarez bado anatazamwa kama moja ya ma-legend wa majogoo wa Merseyside huku mashabiki wa timu hiyo wakitamani siku moja nyota huyo arejee kwenye dimba la Anfield.
Kwahiyo mazungumzo kati yake na Carragher yatawafanya mashabiki wa Liverpool wahisi huenda ndoto yao ikatimia siku moja kwasababu star huyo kuitaja Liverpool kama ndiyo klabu pekee ambayo atarudi siku moja kucheza endapo atarudi England.
Suarez pia amesema anatamani kucheza kwenye klabu ya Ajax ili kuwashuru miamba hao wa Uholanzi kwa yote waliyomfanyia.
Kwasasa anamiaka 29, ni vigumu kwake kucheza kwenye vilabu vingine viwili wakati huo bado anamkataba na klabu ya Barcelona.
Carragher: Inawezekana usimalizie soka lako Barcelona. Ukifikisha miaka 31 au 32 (kwa sasa Suarez anamiaka 29), utapenda kurudi kwenye ligi ya England? Au utaenda kujaribu kwenye ligi nyingine za bara la Ulaya?
Suarez: Hapana, ningependa kubaki hapa kwa miaka mingine zaidi. Nafahamu sikuzote haiwezi kuwa hivyo. Lakini kama ikitokea narejea England, lazima nitaenda Liverpool. Sitaenda kwenye timu nyingine yeyote.
Na haitakuwa kwasababu ya pesa. Ningependa pia kucheza Ajax kwa mara nyingine kwasababu waliniendeleza na kunifanya nitambulike Ulaya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni