
Ligi ya Uingereza ni mpizani mkubwa wa Barcelona ikilinganishwa na Real Madrid,amesema rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Kilabu
20 za ligi kuu ya Uingereza zitaanza kugawanya kitita cha pauni bilioni
5.136 za matangazo ya moja kwa moja kuanzia msimu ujao.''Timu za ligi ya Uingereza zitakuwa na ubabe wa kifedha kuanzia sasa na tuna wasiwasi,''Bartomeu aliiambia BBC Sports.
Kilabu ya Barcelona inakabiliana na Arsenal katika ligi ya vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.

Kilabu kubwa za Uhispania -Barca na Real Madrid,zilijadili kuhusu mikataba yake ya mechi za ligi hiyo zinazoonyeshwa moja kwa moja katika runinga lakini sasa zimezuia kufanya hivyo kupitia sheria mpya ya Uhispania.
0 maoni:
Chapisha Maoni