
Mashabiki wa kilabu
Trabzonspor wamefanya maandamano wakimuunga mkono mchezaji mmoja ambaye
alipewa kadi nyekundu kwa kumuonyesha kadi nyekundi refa.
Salih
Dursun alibeba kadi nyekundu na kumuonyesha refa Deniz Bitnel na kuwa
mchezaji wa nne wa Trabzonspor kutolewa nje katika mbapo kilabu hiyo
ilishindwa 2-1 na Galatasaray.Hatahivyo,amepata ufuasi kwa hatua yake,huku Bitnel akikosolewa kwa mchezo wake.
Trabzonspor pia imeanza kuuza fulana zinazomuonyesha Dursun akifanya kitendo hicho.

Na huku mashabiki wa kilabu hiyo wakibeba kadi nyekundu wakiandamana huko Trabzon,mashabiki katika jimbo la magharibi la Koceli wamewasilisha malalamishi ya uhalifu kwa utumizi m'baya wa mamlaka na kuchochea chuki.
Tranzospor walikuwa chini na wachezaji tisa huku ikiwa mabao ni 1-1 wakati refa Bitnel alipompatia kadi nyekundu Luis Cavandi kwa kucheza visivyo mbali na kuizawadi Galatasaray mkwaju wa penalti.

0 maoni:
Chapisha Maoni