Mwanamfalme ataka uchaguzi wa Fifa Kuahirishwa


 
Mwanamfalme Ali al-Husein
Mawakili wanaomuakilisha mgombea wa urais wa Fifa mwana mfalme Ali bin al-Husein wamesema wamewasilisha ombi lao rasmi la kutaka uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Ijumaa kuhairishwa.
Mwana mfalme Ali, mwenye umri wa miaka 40, amesema hafurahishwi na mipango ya upigaji kura na amewasilisha kesi yake kwa mahakama ya kutatua maswala ya michezo.
Mgombezi huyo kutoka Jordan, aliomba sehemu za kupiga kura kuwa za uwazi , ombi ambalo tume ya kimataifa ya uchaguzi wa soka limepinga.
 
Fifa
Mwana mfalme Ali ni mmojawapo wa wagombea wengine watano wanaotaka kumrithi Sepp Blatter, ambaye anang'atuka mamlakani baada ya miaka 18.
Ali anakabiliana na Jerome Champagne, Gianni Infantino, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na Tokyo Sexwale katika kinyang'anyiro cha kuwania urais wa FIFA.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni