Juhudi za Kenya za kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini katika riadha hazitoshi.
Shirikisho
linapopigana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini katika
michezo (Wada) limekashfu rasimu ya mswada wa sheria uliopendekezwa na
serikali ya Kenya kwa minajili ya kupambana na ongezeko la idadi ya
wanariadha wanaopatikana na hatia ya kutumia madawa hayo.Shirikisho hilo linasema kuwa rasimu hiyo ya sheria haiafikiani na vipengee sheria zake.
WADA imeipa Kenya makataa ya hadi Aprili tarehe 5 kuhakikisha imeanisha sheria zake na kanuni zote za kupambana na madawa yaliyopigwa marufuku.
''Hadi kufikia leo, rasimu ya sheria iliyopendekezwa na serikali ya Kenya na kamati iliyoundwa ilikupambana uenezi wa madawa hayo marufuku ya Kenya, kwa hakika haiafikiani kabisa na kanuni za WADA'' taarifa hiyo ilisema.
Waziri wa michezo wa Kenya bwana Hassan Wario aliiahidi WADA kuwa mapendekezo ya sheria hiyo ya kupambana na matumizi ya madawa yatajadiliwa bungeni na kupitishwa kesho.
Onyo hilo la WADA linatia wasiwasi kwa maelfu ya mashabiki wa riadha nchini Kenya kwani rais wa shirikisho la riadha duniani Lord Sebastian Coe alikuwa ameonya kuwa hatachelea kuipiga marufuku Kenya kutoshiriki mashindano ya Olimipiki yatakayoandaliwa mjini Rio de jenairo Brazil mwezi Agosti mwaka huu.
Kenya ndio mabingwa wa riadha duniani.
Juma lililopita BBC iliripoti kuwa Kenya ilikuwa imeshindwa kuafikia vigezo vilivyowekwa na shirikisho hilo la WADA.
Hadi kufikia sasa takriban wanariadha 40 wamepatikana na hatia ya kutumia madawa yaliyopigwa marufuku.
0 maoni:
Chapisha Maoni