CHAN: Mali 0-0 Ivory Coast


 
Mali 0-0 Ivory Coast
Mabingwa wa Afrika Ivory Coast wanakibarua kigumu dhidi ya wapinzani wao wa jadi Mali wanaopepetana nao sasa hivi katika uwanja wa kitaifa wa Rwanda katika mechi ya pili ya nusu fainali ya kuwania ubingwa wa CHAN mwaka wa 2016.
The Elephants, ambao kwa miaka miwili walishindwa kutamba katika mashindano haya yanayoandaliwa kila baada ya miaka miwili sasa wameimarika hususan baada ya kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mwaka uliopita.
Timu hiyo ilijihakikishia nafasi hii ya nusu fainali baada ya kuilaza Cameroon 3-0 katika hatua ya robo fainali.
Kipindi cha kwanza kimemalizika kwa matokeo ya 0-0.Kila timu inetengeneza nafasi za kufunga magoli.
Dakika ya 11 mkwaju wa Ivory Coast uliishia kwenye mlingoti wa lango na dakika ya 31 Mali walipata penalti, kipa wa Ivory Coast akaipangua.
Kipa ALI BADRA aliokoa mkwaju wa Coulibaly
Wakiwa chini ya kocha wao mpya Michel Dussuyer, Ivory Coast wamethibitisha kuwa wao ni kidedea haswa baada ya kuinyamazisha Gabon 4-1.
Mali kwa upande wao walijikatia tikiti ya nusu fainali baada ya kuisakama bingwa mtetezi Tunisia 2-1.
Hii ndio mara yao ya kwanza kwa Mali kufuzu kwa hatua hii.
The Eagles wanawategemea Mamadou Sissoko na Aly Malle, kupambana na the Elephants katika mechi yao ya 33 baina yao.
Mshindi kati yao anatarehe dhidi ya Leopards ya Congo DR ambaye ilitamausha Guinea mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti hapo jana.
Fainali itaandaliwa siku ya jumapili.
Miongoni mwa wale wanaoshuhudia mechii hii ya kukata na shoka ni wagombea wa kiti cha urais wa FIFA Tokyo Sexwale, Gianni Infantino na Jerome Champagne.
Watatu hao wameketi pamoja katika uwanja huo wa Stade de Kigali .
Kuwepo kwao huko Rwanda kumetokana na habari za kuaminika kuwa shirikisho la soka barani Africa linaandaa mkutano wa wenyeviti wa mashirikisho ya kandanda wa mataifa wanachama.
Mkutano huo wa Ijumaa usiku unapangiwa kutoa mwelekeo wa ni mgombea yupi watakayemuunga mkono katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari tarehe 26.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni